Saturday, March 9, 2013

TAMASHA LA KIHISTORIA LILOWAKUSANYA WAIMBAJI WAKONGWE WA ZAMANI NI TAREHE 17/3/2013 KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE

Lile tamasha la kihistori ambalo limewakusanya waimbaji binafsi , kwaya na bendi kongwe sasa zimebakia wiki mbili kuweza kufanyika ni tarehe 17/3/2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia saa 7:00 mchana hadi saa 12:00 jioni. Watu  na wadau wa muziki wa injili wanaombwa wasipitwe na tukio jili muhimu bali wajitokeze kwa wingi kuwapa ushirikiano waimbaji wetu wa zamani.

Hili ni Tamasha ambalo limeandaliwa kutambua mchango wa wakongwe wa muziki wa injili Tanzania katika kuinua na kuendeleza muziki wa injili nchini. Baadhi ya wakongwe watakao tumbuiza siku hiyo ni:

Nunu na mumewe Donisi Nkone ambao ni waimbaji wakongwe wa muziki wa injili waishio na kuhudumu nchini Marekani

Upendo Kilahiro ambaye pia ni mkongwe wa muziki wa injili na kipenzi cha watu atashambulia katika jukwaa la Tamasha la wakongwe wa muziki injili

Joge Jabili yule muimbaji bonge wa lulu kwaya ataongoza safu nzima ya mashambulizi ya kwa kwaya ya Lulu Mtoni Kwaya ambayo ni moja ya kwaya kongwe kabilsa nchini Tanzania iliyowahi kutamba na wimbo wao wa Lulu. Kumbuka OOOOO Lulu, OOOOO lulu, OOOOO lulu iko mbinguni!!! Wimbo wa Lulu utapigwa live siku hiyo,

Wakitokea nchini Marekani ambapo wamekaa miezi mingi New Life Band chini ya kiongozi wao HONDO ambaye ni muimbaji na mpiga gitaa la bass katika band hiyo, wataimba live katika Tamasha la wakonwe wa muziki wa injili Tanzania

Pastor Safari ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa matamasha ya muziki wa injili Tanzania kutoka DPC Kinondoni pia atashiriki katika Tamasha hili.

Mtaalamu na mtuzi bora wa muziki wa injili Tanzania John Shaban pia atashiriki katika Tamasha hili.

No comments:

Post a Comment