Saturday, March 16, 2013

UPONYAJI NA UKOMBOZI KILUVYA - GOGONI

Hall Johnson kutoka nchini Marekani akishirikiana na mwenyeji wake Apostle John Komanya pamoja Mwinjilist John Shabani watahubiri injili na kufanya maombi ya uponyaji kwa wenye shida mbalimbali jijini Dar es salaam.

Wewe mkazi wa Dar es Salaam na mahali pengine popote Tanzania na duniani unakaribishwa.

Friday, March 15, 2013

GOSPEL CELEBRATION CONCERT

Kutakuwa na Tamasha Kubwa la Kusifu na Kuabudu yaani GOSPEL CELEBRATION CONCERT lililo andaliwa na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu cha St.Mary`s (ST.MARY`S TEACHER`S COLLEGE) kilichopo Tabata,wakishirikiana na vijana wa kanisa la Dar Calvary Temple (DCT), Jumapili hii ya Tarehe 17/03/2013.

Tamasha hili litaanza saa 11 jioni na kumalizika saa 4 usiku. Hakuna kiiingilio yaani bureee kabisa.

Gospel Celebration Concert litapabwa na Waimbaji wafuatao
Maombezi kwa wenye shida yatafanyika..nyote mnakaribiswa sana!.

KUMBUKA HAKUNA KIINGILIOOOOOOO.

Thursday, March 14, 2013

UZINDUZI WA ALBAM IITWAYO MALIPO TOKA KWA MCH JOSHUA MAKONDEKO

Tarehe 24/3/2013 Jumapili. Waimbaji Sifa John, Masanja Mkandamizaji, Mama Mchungaji Josephin Mwasulama, Joseph Nyuki, Enock Johnasy watakupa nyimbo nyingi zenye kuleta uwepo wa Bwana.

Hii albam iitwayo MALIPO ni albam inayofuata ile ya ZA MWIZI AROBAINI utafanyika pale CITY HARVEST siku ya Jumapili Tarehe 24 March, 2013

Sunday, March 10, 2013

ZIMA UKIMYA NA JESSICA HONORE


Kongamano la Zima Ukimya na Jessica Honore. Hili ni kongamano litakalofanyika ndani ya CITY CHRISTIAN CENTER, Dar es Salaam, Tanzania. Mambo yatakayofanyika katika kongamano la Zima Ukimya na Jesca Honore ni Live Album Sumling, Ministry (The Jessica Music) Preview, Praise and Worship Moment, Uchangishaji fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya muziki na mambo mengine  mengi.

Waimbaji waalikwa watakao pamba na kuhudumia kongamano hili ni Miliam Lukindo Wa Mauki pamoja na Upendo Kilahiro, Vocapela, Holy Bass Getor, Doxsaz, Glorious Celebration, R.T.M Bank na wengine wengi




Kwa kiasi kidogo cha fedha ambacho ni shilingi 15,000/= za kitanzania unaweza kuhudhuria kongamano la la Zima Ukimya na Jesca Honore na kupata nafasi ya kushiriki kusongesha mbele kazi ya Bwana na kukutana na wasanii na watu wengine mbalimbali watakao hudhuria kongamano hilo.

Tiketi za tamsha hilo zinapatikana Praise Power Radio na katika kanisa la Word Alive Centre Sinza Mori au unaweza kupiga simu namba hizi 0718 807278 na 0712 332007

Unakaribishwa sana!